Je, BreastScreen SA ni nini?
BreastScreen SA inatoa uchunguzi wa matiti (Eksrei ya matiti) bila malipo kila baada ya miaka miwili, hasa kwa wanawake wenye umri wa miaka 50 hadi 74.
Uchunguzi wa matiti unaweza kubaini saratani ya matiti mapema, mara nyingi kabla ya dalili kujitokeza. Saratani ya matiti inapogunduliwa mapema, inakuwa rahisi zaidi kuitibu.
BreastScreen SA ni tawi la Australia ya Kusini la BreastScreen la Australia linalotambulika, yaani mpango wa kitaifa wa kuchunguza saratani ya matiti ya wanawake bila dalili za saratani ya matiti, na limekuwa likitoa huduma tangu mwaka wa 1989.
Uchunguzi wa matiti ni bure, na hauhitaji rufaa ya daktari ili kuweka miadi.
Je, unafahamu kuhusu uchunguzi wa bila malipo wa saratani ya matiti?
Je, uchunguzi wa matiti ni nini?
Uchunguzi wa matiti ni picha ya matiti ya mammogram ya uchunguzi (kiwango cha chini cha kipimo cha Eksirei ya matiti), kwa wanawake ambao hawana dalili za matiti kama vile uvimbe, chuchu kutoa uchafu, au mabadiliko kwenye matiti ambayo si ya kawaida.
Picha ya matiti ya uchunguzi wa mammografia inajumuisha kupiga angalau picha mbili ya kila titi - moja kwa juu na moja kwa pembeni. Kwa sasa ndiyo uchunguzi unafaa zaidi kwa saratani ya matiti isiyogunduliwa.
Ikiwa mwanamke ana dalili ya matiti, anaweza kuhitaji uchunguzi wa picha ya matiti ya mammogram ya kugunduliwa. Picha ya matiti ya mammogram ya kugunduliwa inahusisha picha ya kina zaidi ya matiti ili kuwawezesha madaktari kutathmini dalili. Baadhi ya saratani hazionekani kwenye picha ya matiti ya mammogram, hivyo vipimo vingine vya kina vinaweza kuhitajika.
Hii ndio sababu uchunguzi wa matiti unafaa tu kwa wanawake ambao hawana dalili za matiti.
Nani anaweza kufanyiwa uchunguzi wa matiti?
BreastScreen SA inawaalika wanawake wenye miaka 50 hadi 74 kuchunguzwa matiti kila baada ya miaka miwili. Ushahidi unaonyesha uchunguzi wa kawaida unafaa zaidi katika rika hili.
Wanawake wenye umri wa miaka 40 hadi 49 na miaka zaidi ya 75 pia wanaweza kuweka miadi ya uchunguzi wa matiti bure, lakini wanahimizwa zaidi kuzungumza na daktari wao wanapoamua kama uchunguzi wa matiti ni sahihi kwao.
Uchunguzi wa matiti sio uchunguzi mzuri kwa wanawake chini ya miaka 40. Japokuwa saratani ya matiti inaweza kutokea katika umri wowote, ni mara chache sana kwa wanawake wenye miaka chini ya 40.
Wanawake ambao wana historia thabiti ya familia kuugua saratani ya matiti wanaweza kupimwa saratani kila mwaka kuanzia miaka 40.
Kwa taarifa za uchunguzi kwa rika tofauti na kwa taarifa za historia thabiti ya familia, bonyeza hapa.
Je, BreastScreen SA inafaa kwako?
Baadhi ya wanawake wanaweza kuhitaji uangalizi na huduma tofauti ambazo siyo sehemu ya uchunguzi.
Hii inajumuisha wanawake ambao:
- wana dalili za matiti (kama vile kuvimba, chuchu kutoa uchafu au mabadiliko kwenye matiti yake)
- wana historia thabiti ya familia kuugua saratani ya matiti na/au saratani vya uzazi
- waligundulika kuwa na saratani ya matiti katika miaka mitano iliyopita
- wamekakamaa sehemu ya juu ya mwili au wanashindwa kushikilia au kuhimili uzito wao wenyewe.
Zungumza na daktari wako au wapigie simu BreastScreen SA kwa namba 13 20 50 ili kuhakikisha kuwa unapata uangalizi na huduma inayokufaa zaidi.
Je, niende wapi kwa ajili ya miadi ya uchunguzi wa matiti?
BreastScreen SA ina kliniki 8 za kudumu ndani ya eneo la mji mkuu wa Adelaide, na vituo vitatu vinavyotembea ambavyo vinatembelea vijijini, maeneo ya mbali, nje ya mji mkuu na baadhi ya maeneo ya mji mkuu kila baada ya miaka miwili. Maeneo ya kliniki zetu za kudumu zimeorodheshwa nyuma ya kijitabu hiki, na orodha kubwa ya maeneo inaweza kupatikana hapa.
Je, niombaje miadi na BreastScreen SA?
Unaweza kuwapigia simu BreastScreen SA kwa namba 13 20 50 ili kupanga miadi yako kati ya saa 2.30 asubuhi na saa 11 jioni. Tafadhali kumbuka kwamba tutahitaji kukuuliza maswali kadhaa ya afya binafsi unapoweka nafasi, hivyo hakikisha una muda na kuwa sehemu ya faragha ili kujibu maswali hayo unapopiga simu.
Vinginevyo, unaweza kuweka nafasi ya miadi hapa.
Je, nini kitatokea kwenye miadi yangu?
Tafadhali fika kabla ya dakika 10 kwenye miadi yako ili kujipa muda wa kutosha wa kujaza fomu yako ya idhini na kuuliza maswali. Tafadhali pia kumbuka kuja na kitambulisho chako cha Medicare.
Mmoja wa wahudumu wetu wa mapokezi wakarimu watahakikisha jina lako kamili, tarehe ya kuzaliwa na anwani yako pamoja na wewe ili kuhakikisha ni sahihi na kwamba tunamchunguza mtu sahihi. Kisha mtaalamu wa kike wa picha za Eksirei aliyebobea atakuchukua kuelekea kwenye chumba cha uchunguzi na utatakiwa kuvua nguo kuanzia kiunoni kwenda juu. Unaweza kuweka shati au fulana yako juu ya mabega yako kama utapenda, au magauni ya kutupwa baada ya matumizi yanapatikana ukiyaomba.
Utapokuwa tayari, mpiga picha za Eksirei ataweka titi moja baada ya lingine kwenye mashine ya mammografia ya matiti. Mashine itagandamiza kwa nguvu kwenye titi lako kwa sekunde 10 hadi15 ili kupiga picha. Kwa kawaida picha mbili za kila titi zitapigwa, moja kwa juu na moja kwa pembeni. Wanawake wenye matiti makubwa wanaweza kuhitaji picha za ziada ili kuhakikisha tishu zote za titi zinaweza kuonekana. Mara baada ya picha zako kupigwa, utaweza kuvaa nguo na miadi yako itakuwa imeisha.
Picha zako hazitakuwa tayari wakati wa miadi yako. Mpigapicha za Eksirei aliyekupiga picha za mammogram ya matiti ataangalia ubora wa kiufundi wa picha zako. Kisha picha zako zitatumwa kwenda Kitengo chetu cha Uratibu cha Taifa huko Adelaide ambako zitasomwa na angalau wataalam wawili wa picha za mionzi.
Je, uchunguzi wa matiti unaumiza?
Wanawake wengi wana wasiwasi kwamba uchunguzi wa matiti utakuwa unaumiza. Ukweli ni kwamba kila mwanamke yuko tofauti. Wengine wanasema haufai, wengine wanasema unauma kiasi, na wengine wameripoti kwamba hakuna shida kabisa. Ikiwa unajisikia usumbufu ujue kuwa itaisha kwa sekunde chache tu. Hii ni kwa sababu matiti yako yanapaswa kugandamizwa kwa nguvu katika mashine ya Eksirei ili picha iweze kupigwa vizuri. Ikiwa utahisi kuuma sana, unaweza kusitisha utaratibu huo wakati wowote. Tafadhali zungumza na mpiga picha za Eksirei wakati wa miadi yako ikiwa una wasiwasi.
Je, kuna hatari za mionzi?
Kila wakati unapopigwa picha za mammogram ya matiti, unawekwa kwenye kiwango kidogo sana cha mionzi. Vitengo vya picha za Eksirei ya matiti vinatumia kiwango kidogo sana cha mionzi iwezekanavyo ili kupiga picha zenye ubora mkubwa. Kiwango cha mionzi ni sawa na eksirei nyingine nyingi ambazo watu wanapigwa, na kinapunguzwa zaidi kwa mgandamizo wa matiti. Utafiti unaonyesha kwamba faida ya uchunguzi wa saratani ya matiti unazipita hatari za mionzi.
Je, matokeo yanaamuliwaje?
Baada ya uchunguzi wa matiti yako, picha zako zitasomwa na wataalamu huru wa picha za mionzi angalau wawili. Kutegemeana na ugunduzi wao, utapewa matokeo mojawapo: ama 'hakuna ushahidi wa saratani ya matiti' au 'kuitwa kwa ajili ya vipimo zaidi'.
Kwa kawaida matokeo hutumwa kwako na daktari wako aliyeteuliwa ndani ya siku 14 za miadi. Ikiwa kipimo hiki ni kwa ajili ya kuchunguza saratani ya matiti pekee, mabadiliko yoyote yasiyo ya saratani (yasiyo hatari) hayatolewi taarifa.
Je, inakuwaje iwapo nahitaji vipimo zaidi?
Karibu 5% ya wanawake waliochunguzwa wataombwa kurudi tena BreastScreen SA kwa ajili ya vipimo zaidi. Hii haimaanishi kwamba una saratani ya matiti, lakini wakati mwingine vipimo zaidi vinahitajika ili kuhakikisha. Hii inatokea mara nyingi zaidi kwa wanawake waliofanyiwa uchunguzi kwa mara ya kwanza, kwani hakuna picha za awali za mammogram ya matiti za kulinganisha. Kitu ambacho kinaweza kuonekana si cha kawaida katika upigaji picha za mammogram ya matiti wa kwanza unaweza kuwa wa kawaida kabisa.
Wanawake wanakaribishwa tena kwenye Kliniki yetu ya Utathmini iliyojitolea huko Adelaide, ambako watachukuliwa vipimo, ambavyo vitajumuisha taarifa za kina za picha za eksirei ya matiti, picha za mawimbi ya sauti, uchunguzi wa matiti wa kitabibu, na katika hali fulani biopsi. Hii inaweza kuwa hali ya kuogofya zaidi na timu yetu ya wataalamu wa afya watahakikisha unajisikia vizuri wakati wa ziara yako.
Wanawake wengi ambao hufanyiwa vipimo zaidi wanahakikishiwa kwamba hawana saratani ya matiti. Kisha wanaalikwa tena kwa ajili ya uchunguzi unaofuata wa matiti muda unapowadia.
Je, itakuwaje ikiwa nina saratani ya matiti?
Idadi ndogo ya wanawake (chini ya 1% ya wanawake wa Australia ya Kusini waliochunguzwa) watakutwa na saratani ya matiti baada ya miadi yao ya Kliniki ya Utathmini. Timu ya wataalamu wa afya watakuongoza katika mchakato huu na kukueleza nini kitatokea baadae.
Kwa kuwa BreastScreen SA haiwatibu wanawake wa saratani ya matiti, tutakusaidia kupanga mahitaji yako ya matibabu ya baadaye kwa kuwasiliana na daktari wako. Daktari wako atajadili na wewe kuhusu rufaa yako kwa daktari bingwa, matibabu na machaguo ya ufuatiliaji.
Kwa maelezo zaidi ya saratani ya matiti, unaweza kutembelea tovuti ya Cancer Australia.
Je, mambo gani ni ya hatari kwa saratani ya matiti?
Kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kuongeza hatari yako ya kupata saratani ya matiti. Haya yanajumuisha mambo binafsi kama vile kuwa mwanamke, umri wako, ikiwa awali uligundulika kuwa na saratani ya matiti, uzito wa matiti yako na historia ya familia yako. Mambo mengine ni mfumo wa maisha kama vile lishe yako, mara ngapi unafanya mazoezi, ikiwa unavuta sigara au unakunywa pombe mara kwa mara. Ikiwa unataka kutathmini hatari yako, unaweza kuzungumza na daktari wako au kutumia maswali yafuatayo ya mtandaoni kwenye www.breastcancerrisk.canceraustralia.gov.au.
Je, uzito wa matiti ni nini?
Matiti ya mwanamke yameumbwa kwa tishu za mafuta na tishu za tezi ndogo za nyuzinyuzi (tishu zisizo za mafuta). Kwenye picha za mammografia ya matiti, tishu za mafuta zinaonekana nyeusi ili hali tishu zilizobaki za matiti zinaonekana nyeupe au 'nzito'. Kiasi kinachofaa cha tishu ya tezi ndogo za nyuzinyuzi (sehemu nyeupe) kwenye picha za mammogram ya matiti inajulikana kama uzito wa matiti.
Kwani saratani ya matiti pia inatokea kama sehemu nyeupe kwenye picha za mammografia ya matiti, uzito mkubwa wa matiti unapunguza kiwango cha urahisi wa kufaa wa uchunguzi wa picha za eksirei. Ingawa ni hivyo, uchunguzi wa picha za matiti za eksirei bado ni uchunguzi mzuri zaidi wa saratani ya matiti kwa wanawake wenye miaka 50 hadi 74 kulingana na idadi ya watu, ikiwemo wale wote wenye matiti mazito.
Matiti mazito ni kawaida na hasa hutokea karibia 40% ya wanawake wenye miaka zaidi ya 40.
Uzito wa matiti yako utaripotiwa na matokeo ya uchunguzi wa matiti.
Bonyeza hapa ili kupata maelezo zaidi kuhusu uzito wa matiti.
Je, nini faida ya uchunguzi wa matiti wa mara kwa mara?
Kugundua saratani ya matiti mapema
Mwaka 2008, utafiti wa ndani umebaini kwamba wanawake wa Australia ya Kusini wenye miaka 50 hadi 69, ambao wanafanyiwa uchunguzi wa matiti kila baada ya miaka miwili, walipunguza uwezekano wa kufa kutokana na saratani ya matiti kwa hadi 41%.*
Matibabu ya kupunguza kusambaa
Kwa kila wanawake 1000 waliofanyiwa uchunguzi wa matiti, wanawake 6 tu watakutwa na saratani ya matiti. Saratani za matiti zilizogunduliwa na BreastScreen SA hasa ni ndogo zaidi, inayofanya ziwe rahisi zaidi za kutibu. Matokeo ya afya ya mwanamke kwa ujumla huimarika.
Hakikisho
Wanawake wengi ambao wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti watapata matokeo 'hakuna ushahidi wa saratani ya matiti' na watajisikia kuwa na imani kuwa wamechukua tahadhari ya kutosha katika kulinda afya zao za matiti.
Je, mapungufu na hatari za uchunguzi wa matiti ni zipi?
Wakati uchunguzi wa picha za matiti za mammografia kwa sasa ndio njia inayofaa zaidi kwa uchunguzi wa saratani ya matiti, kuna mapungufu unayotakiwa uyafahamu.
Saratani ya matiti ipo lakini haijabainika
Uchunguzi wa picha za mammogram ya matiti hautagundua saratani zote za matiti. Baadhi ya saratani haziwezi kuonekana kwenye uchunguzi wa picha za eksirei ya matiti au zinaweza kuanza katikati ya wakati wa upigaji picha za mammogram ya matiti. Kuna uwezekano mdogo kwamba saratani inaweza kukosekana kwenye uchunguzi wa picha za mammogram ya matiti. Hii inaweza kusababisha kukutwa na saratani ya matiti baadaye.
Chini ya mwanamke 1 kati ya 1000 wenye miaka 50 hadi 74 watakutwa na saratani ya matiti katika kipindi cha miezi 12 kufuatia uchunguzi wao wa matiti.
Sababu nyingine zinazochangia ufanisi wa picha ya matiti ya mammogram zinaweza kujumuisha umri wa mwanamke na uzito binafsi wa matiti.
Saratani ya matiti imekutwa na kutibiwa isivyofaa (utambuzi uliopitiliza)
Uchunguzi wa matiti pia unaweza kubaini saratani ya matiti ambayo inawezekana kutokuwa hatari kwa maisha. Hii inamaanisha mwanamke anaweza kuchagua kutibiwa saratani ambayo haiwezi kuwa na madhara kwako, japokuwa matibabu yenyewe yanaweza kusababisha madhara kwake.
Bado haiwezekani kusema ni saratani gani ya matiti hasa inayoweza kuwa hatari kwa maisha na ipi ambayo haiwezi kuwa hatari.
Vipimo vya ziada vinafanyika, lakini saratani ya matiti haibainiki
Ikiwa eneo lenye tatizo au mabadiliko kwenye tishu ya titi lako imegundulika kwenye uchunguzi wa picha za mammogram ya matiti, utaitwa tena kwenye Kliniki ya Utathminii ya BreastScreen SA kwa ajili ya vipimo zaidi. Vipimo hivi vitajumuisha picha zaidi za mawimbi ya sauti za matiti za mammogram, na ikiwezekana uchunguzi wa matiti wa kitabibu au biopsi. Kwa kuwa muda huu unaweza kuwa wa hofu kwa wanawake, wengi wao watahakikishiwa kuwa hawana saratani ya matiti.
Je, kwa nini uelewa wa matiti ni muhimu?
Hata kama unachunguza matiti kila baada ya miaka miwili, bado ni muhimu kuwa na uelewa wa matiti kwa sababu saratani ya matiti inaweza kuanza wakati wowote. Hii inajumuisha muda wa katikati ya miadi ya uchunguzi.
Ni muhimu kujua muonekano wa kawaida na hisia ya matiti yako. Vitu unapaswa kuviangalia ni pamoja na:
- uvimbe mpya au bongebonge kwenye matiti yako, hasa ikiwa katika titi moja tu.
- kubadilika ukubwa na umbile wa titi lako
- mabadiliko kwenye chuchu kama vile utando, kidonda, wekundu au chuchu kujivuta kwa ndani
- kutoka uchafu kwenye chuchu yako ambako kunatokea bila kuminya chuchu
- madadiliko kwenye ngozi ya chuchu yako kama vile wekundu au kubonyea au kukunjamana kwa ngozi
- maumivu yasiyoisha.
Mabadiliko mengi ya matiti yanaweza yasiwe kwa sababu ya saratani ya matiti lakini unapaswa kuyachunguza ili kuwa na uhakika. Ikiwa utabaini mabadiliko katika muonekano au hisia ya matiti yako, hata kama uchunguzi wako wa picha za matiti za mammogram ulikuwa kawaida, mwone daktari wako bila kuchelewa.
Mapendekezo mazuri ili kuifanya ziara yako iwe rahisi na nzuri zaidi.
Tafadhali usipake poda ya ulanga au kiondoa harufu siku ya miadi kwa kuwa vinaweza kuathiri uchunguzi wako wa matiti.
- Vaa sketi na blauzi kwa kuwa utatakiwa kuvua sidiria yako na blauzi wakati wa uchunguzi wa matiti.
- Tafadhali kumbuka kuja na Kitambulisho cha Medicare kwenye miadi yako, pamoja na fomu ya idhini iliyojazwa na kusainiwa.
- Tafadhali fika kabla ya dakika 10 ya muda wa miadi yako ili tuweze kushughulikia makaratasi yako.
- Ikiwa umepigwa picha za matiti za mammogram sehemu yoyote ile, tafadhali wajulishe wafanyakazi wetu wakati wa kuweka nafasi ya miadi yako.
- Ikiwa una maswali yoyote tafadhali waulize wafanyakazi wetu wakarimu.
Viunganishi muhimu, marejeo na maandiko ya ziada
Cancer Australia
Kikokotoo cha hatari ya saratani ya matiti
breastcancerrisk.canceraustralia.gov.au
Taasisi ya Austria ya Afya na Ustawi wa Jamii
Jinsi ya kupanga miadi
Piga simu 13 20 50 au andika maelezo yako kwenye fomu ya kuweka nafasi hapa.
Rufaa ya daktari haihitajiki.
Huduma ya mkalimani wa bure na njia ya kiti cha magurudumu kwa walemavu inapatikana.
Maeneo yalipo kliniki za BreastScreen SA
Vituo vya uchunguzi vinavyotembea
Vituo vyetu vitatu vinavyotembea vinatembelea maeneo ya vijijini, mbali, mji mkuu na nje ya mji mkuu kila baada ya miaka miwili. Tafadhali tembelea tovuti yetu ili kuona maeneo na maelezo ya kutembelea.